ZIARA ZA NJE ZA DKT SAMIA ZAILETEA NCHI TSH BIL 312
ZANZIBAR
Imeelezwa kuwa ziara za nje ya nchi anazozifanya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zimekuwa ni fursa kwa Tanzania kupata fedha kiasi cha shilingi bilioni 312 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uimarishaji wa Sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Tanzania (TASFAM) hatua ambao itainua shughuli za uvuvi na ufugaji wa samaki Tanzania Bara na visiwani.
Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mifugo na uvuvi mbele ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Agosti 20, 2024 kwenye Hafla ya utoaji wa Vyeti kwa wavuvi 96 wa Kizimkazi Kusini Unguja waliopatiwa mafunzo ya Uvuvi endelevu na wa kisasa katika Uwanja wa Mwehe Makunduchi visiwani Zanzibar
Aidha wizara ya mifugo na uvuvi imeongeza kwamba Serikali inapanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 452 kwa ajili ya kuboresha shughuli za ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wa maziwa kwa Tanzania Bara na Visiwani.
