TZ NI MWENYEKITI WA NAIROBI CONVENTION COP BUREAU

 

TZ NI MWENYEKITI WA  NAIROBI CONVENTION COP BUREAU

TZ NI MWENYEKITI WA  NAIROBI CONVENTION COP BUREAU

MADAGASCAR
Tanzania imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Nairobi (Nairobi Convention-COP Bureau) baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wakati wa mkutano wa 11 uliofanyika  Agosti 20 hadi 22, 2024 Antananarivo, Madagascar na kuchukua nafasi hiyo kutoka Madagascar na itaitumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili hadi 2026.
Jukumu la Tanzania kama Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mkataba wa Nairobi ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mkataba huo, kufanya maamuzi mbalimbali yanayohitajika kwa Sekretarieti ya Mkataba wa Nairobi na kuongoza mikutano yote inayohusisha nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi.
Nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi ni pamoja na Kenya, Tanzania, Msumbiji, Comoro, Madagascar, Seychelles, Somalia na Sudan Kusini, huku kila nchi mwanachama ikichangia mikakati ya uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani kwa kushirikiana na nchi nyingine za kikanda.
Mkataba wa Nairobi ulianzishwa chini ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) na unalenga kushughulikia masuala kama vile uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali za baharini.