SERIKALI YAWAGUSA WAVUVI MKOANI MARA MKOPO WA VIZIMBA

 

SERIKALI YAWAGUSA WAVUVI MKOANI MARA MKOPO WA VIZIMBA

 SERIKALI YAWAGUSA WAVUVI MKOANI MARA MKOPO WA VIZIMBA

MARA
Serikali imetoa kiasi cha shilingi 117 kwa Chama cha Ushirika cha Uvuvi Busumi   (wanachama 20) Mkoani Mara wanaofanya shughuli zao katika ziwa Victoria kwa ajili ya kununua vizimba vinne, kununua vifaranga vya samaki, chakula na bima kwa ajili ya ufugaji wao wa samaki, hatua hii ikiwa ni jitihada za kuendeleza sekta ya uvuvi nchini.
Hadi hivi sasa tayari Wataalamu wamekamilisha kazi yao, na vizimba vimeshawekwa kwenye maji (Ziwa Victoria) katika eneo la kijiji cha Suguti
Aidha Wavuvi wa Busumi  wanatoa shukurani zao za dhati kwa Serikali chini ya uongozi bora wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mikopo kuboresha uvuvi wao wa kisasa ili kupata kipato cha juu
USIPITWE:- Mapema mwaka huu, Dkt Samia alisisitiza dhamira ya serikali yake ya kuimarisha sekta ya uvuvi nchini ili kuongeza mchango wake katika pato la taifa.