TSH MIL 800 ZAWAPATIA HOSPITALI NYASA
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi milioni 800 ili kujenga Hospitali ya wilaya Nyasa iliyopo Mkoani Ruvuma lengo likiwa ni kusogeza na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ambao awali walilazimika kwenda nje ya wilaya hiyo kufuata matibabu.
Hospitali ya Wilaya ya Nyasa inatoa huduma zote muhimu kwa wananchi wa Mbambabay na wilaya ya Nyasa kwa ujumla.
Kabla ya hospitali hiyo wananchi wa wilaya ya Nyasa walikuwa wanasafiri umbali wa zaidi ya kilometa 66 kufuata huduma za matibabu katika Hospitali ya Mbinga.