TSH BIL 60.144 KUJENGA KM 33.61 IRINGA
IRINGA
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetoa kiasi cha shilingi bilioni 60.144 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo) kwenda wilaya ya Kilolo kilometa 33.61 kwa kiwango cha lami mradi unaotekelezwa na Mkandarasi China Henan Engineering Company.
Mradi huu ni moja ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia kupitia Program ya Roads to Inclusion and Social Economic Opportunities (RISE), ambapo kukamilika kwa barabara hii italeta ufanisi mkubwa katika Sekta ya Usafirishaji katika maeneo hayo.
