HALI ILIVYO SASA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.
TANZANIA
Serikali imeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika ngazi mbalimbali za utoaji wa huduma za afya nchini.
Hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umefikia wastani wa 81% katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya ambapo kwa Zahanati imefikia 77%, Vituo vya Afya 71%, Hospitali za Halmashauri 73%, Hospitali za Rufaa za Mikoa 99% na Hospitali za Rufaa za Kanda, Maalumu na Taifa 86%.
