SERIKALI KUNUNUA BOTI ZINGINE 240 ZA UVUVI

 

SERIKALI KUNUNUA BOTI ZINGINE 240 ZA UVUVI

SERIKALI KUNUNUA BOTI ZINGINE 240 ZA UVUVI

ZANZIBAR
Serikali ya awamu ya sita inatarajia kununua boti zingine za kisasa za uvuvi zipatazo 240  na kutolewa kwa wavuvi  hatua itakayoongeza idadi ya boti  za mwanzo 160 ambazo zilikopeshwa kwa wavuvi  989 kutoka katika maeneo mbalimbali nchini.
Taarifa kutoka wizara ya mifugo na uvuvi inasema kiasi cha fedha shilingi bilioni 321 kutoka kwenye mradi wa uimarishaji wa  Sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Tanzania (TASFAM) miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na fedha hizo ni pamoja na ununuzi wa boti hizo za kisasa ambazo zitagawiwa kwa wavuvi wa Tanzania Bara.
ZINGATIA:- Serikali imejipanga kukuza sekta ya uvuvi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa meli za kisasa za uvuvi katika bahari kuu, ujenzi wa bandari za uvuvi katika maeneo ya Kilwa Masoko mkoani Lindi na Bagamoyo ili kuongeza pato la taifa.