TSH BIL 33.8 ZABORESHA KIWANJA CHA NDEGE SONGWE

 

TSH BIL 33.8 ZABORESHA KIWANJA CHA NDEGE SONGWE

TSH BIL 33.8 ZABORESHA KIWANJA CHA NDEGE SONGWE

Huu ni uwanja wa ndege wa Songwe ulioboreshwa katika miundombinu yake.
Maeneo ambayo yamefanyiwa maboresho/ ujenzi na upanuzi ni Ujenzi wa sehemu ya kuruka na kutua Ndege "Runways" ambapo umefanyika ujenzi wa tabaka la juu la lami KM 3.3, Ujenzi wa Uzio kuzunguka uwanja KM 10 na Usimikaji wa taa za kuongozea Ndege, pamoja na Jengo la kisasa la abiria.
Miradi yote katika uwanja wa Ndege Songwe imegharimu jumla ya shilingi bilioni 33.8 na kukamilika kwa miradi hiyo inaenda kuifungua zaidi Nyanda za Juu Kusini ambayo ni ukanda muhimu kwa uzalishaji chakula, utalii na lango la kuingia na kutoka nchi jirani za Kusini mwa Afrika.