TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA MASOMO YA SAYANSI
DAR ES SALAAM
Wataalamu kutoka Tanzania na China walikutana jijini Dar es Salaam kutafuta njia bora za kupeleka uvumbuzi na matokeo ya utafiti katika kuendeleza ufundishaji wa masomo ya sayansi.
Mkutano huo wa siku moja uliwakutanisha wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal kutoka China.
Uwepo wa mkutano huo ulikwenda sambamba na dira ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu nchini, ambayo ilisisitiza elimu ya sayansi, hisabati, utafiti na ubunifu.
Aidha UDSM imekuwa ikitenga zaidi ya shilingi bilioni 3 kila mwaka kwa ajili ya utafiti hivyo kuwepo kwa mkutano huo ni matokeo ya utafiti unaofanywa kati ya vyuo vikuu viwili.
Vilevile ushirikiano kati ya UDSM na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal kutoka China kupitia teknolojia ya kidijitali utasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu, kuokoa muda na gharama.
