MANUNGU WAJENGEWA SHULE MPYA
Serikali imekamilisha ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Manungu wilayani Kongwa Mkoani Dodoma kupitia mradi wa SEQUIP.
Ujenzi huo ambao umegharimu shilingi milioni 544.2 unaenda kupunguza adha ya wanafunzi kutembea takribani KM 8 kwenda shule.