MTO RUFIJI KUZALISHA MAJI LITA MILIONI 750
DAR ES SALAAM
Mradi mpya wa Mto Rufiji unatarajiwa kuzalisha lita milioni 750 kwa siku katika awamu yake ya kwanza, huku uwezo wake ukitarajiwa kuongezeka maradufu katika awamu ya pili hatua ambayo itaongeza upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa ya Dar es salaa na Pwani
Hivi sasa, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wanategemea maji ya Mto Ruvu, Mto Kizinga, Mto Wami na visima mbalimbali vya maji, ambavyo kwa pamoja vinazalisha lita milioni 534.6 kwa siku. Kwa mahitaji ya kila siku ya lita milioni 544.
