TANZANIA, JAPAN KUIMARISHA ZAIDI UHUSIANO

 

TANZANIA, JAPAN KUIMARISHA ZAIDI UHUSIANO

TANZANIA, JAPAN KUIMARISHA ZAIDI UHUSIANO 

TOKYO
Tanzania na Japan zimekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa karibu ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Nchi hizo mbili zimefikia makubaliano hayo wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika kati ya Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Tanzania), na Naibu Waziri wa Nchi wa Japan, Kyoto Tsuji, ofisini kwake Tokyo.
Wizara hizo mbili zimekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa karibu ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya pande zote mbili.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Masharaiki ya Tanzania imesema Tanzania imedhamiria kuongeza viwango vya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, na hivyo kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya pande zote mbili.
Nae naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje ya Japan bwana Tsuji amesisitiza utayari wa Japan kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya mataifa yote mawili, na kuongeza kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania na nchi nyingine za Afrika ili kupanua biashara na Bara la Afrika ili kusaidia na kuwezesha maendeleo katika bara.