SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU LINDI VIJIJINI

 

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU LINDI VIJIJINI

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU LINDI VIJIJINI

LINDI
Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu  Mkoani Lindi ( Lindi vijijini) ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo kusafirisha mazao ya kilimo.
Baadhi ya barabara zilizo chini ya mpango huo ni Namkatila, Matambalale A, Matambalale B Namikulo zinazounganisha na barabara ya Nangwego.
Barabara nyingine inaanzia Ruangwa hadi Namichiga, yenye urefu wa kilomita 21 ambayo  itajengwa kwa kiwango cha lami (Barabara hii itajengwa na Wakala wa Barabara nchini -TANROADS).
Aidha Serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ruangwa kwa kiwango cha changarawe kama vile barabara ya  Chikwale-Machang’anja.
Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa barabara ya Namichiga – Namkonjela – Nambilanje-Nanjalu- Kiperemende inayoelekea kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa.