SERIKALI YAWAPA LIPAUMBELE WAHANDISI WANAWAKE
RUKWA
Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuwashirikisha wakandarasi na washauri wazawa hususani wanawake katika miradi ya ujenzi kupitia mkakati wa maudhui ya ndani unaolenga kubakisha sehemu kubwa ya manufaa ya miradi nchini.
Serikali imepiga hatua kubwa katika kuwashirikisha wanawake kwenye tasnia hiyo kwa kutengeneza fursa za kujiajiri, kutoa programu za kufufua kazi na kutoa elimu ya ujenzi katika vyuo vikuu.
Hadi kufikia Julai 2024, kuna wahandisi 38,233 nchini Tanzania, huku 5,006 wakiwa wanawake, ambayo ni takriban asilimia 15.07.