NFRA KUNUNUA TANI 100,000 ZA MAHINDI SUMBAWANGA
RUKWA
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ofisi ya Kanda ya Sumbawanga inatarajia kununua tani 100,000 za mahindi kwa kutumia mfumo mpya wa kidijitali ulioundwa ili kuongeza ufanisi katika shughuli za ununuzi wa nafaka.
NFRA inaruhusu wakulima wadogo, wafanyabiashara wakubwa na vyama vya ushirika kuuza mahindi yao katika vituo mbalimbali vya ununuzi vya Wilaya ya Sumbawanga, vikiwemo Mazwi, Kanondo na Laela.
Vituo vya ziada ni pamoja na Mwimbi, Matai na Mkombo katika Wilaya ya Kalambo, pamoja na Namanyere, Kasu na Ntalamila wilayani Nkasi.
Kwa sasa, NFRA inaendesha vituo 72 vya ununuzi katika mikoa minane, ikiwamo Dodoma, Dar es Salaam (Kipawa), Njombe (Makambako), Songwe, Rukwa (Sumbawanga), Manyara (Babati), Shinyanga na Ruvuma.