MABORESHO MAKUBWA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

 

MABORESHO MAKUBWA MAMLAKA YA  HALI YA HEWA

MABORESHO MAKUBWA MAMLAKA YA  HALI YA HEWA

TANZANIA
Serikali inafanya maboresho makubwa Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) nchini lengo likiwa ni kuongeza ufanisi zaidi kwa mamlaka hiyo.
Baadhi ya miradi inayotekelezwa ili kuboresha TMA ni pamoja ujenzi wa rada mbili ambazo  zitafungwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Dodoma na kufanya jumla ya rada za hali ya hewa nchi nzima kufikia saba.
Pia serikali imesaini mikataba ya uboreshaji wa rada zilizowekwa Mwanza na Dar es Salaam  (Kituo cha Dar es Salaam kinahudumia nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi )
Aidha  Serikali imekamilisha uwekaji wa mitambo ya kufuatilia hali ya hewa katika viwanja vya ndege vya Songwe, Zanzibar, Mtwara, Arusha na Songea huku mitambo ya aina hiyo ikifungwa katika viwanja vya Musoma, Iringa na Mpanda hatua kwa hatua.