SERIKALI KUNUNUA MPUNGA TSH 900 KWA KG

 

SERIKALI KUNUNUA MPUNGA TSH 900 KWA KG

SERIKALI KUNUNUA MPUNGA TSH 900 KWA KG

MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameielekeza wizara ya kilimo kupitia wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kununua kilo ya mpunga kwa shilingi mia 900 kutoka bei ya shilingi 570 ya hapo awali.
Maelekezo hayo ameyatoa Agosti 5,2024 akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ccm Ifakara Mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo aliyoianza Agosti 2 mwaka huu.
Aidha Dkt Samia ametoa onyo kwa viongozi wanaotumia vyeo vyao kuwadhulumu wakulima kwa kununua mazao kwa bei isiyoridhisha na wao kuyauza kwa bei inayoridhisha sokoni.