BONDE LA KILOMBERO KUENDELEZWA

 

BONDE LA KILOMBERO KUENDELEZWA

BONDE LA KILOMBERO KUENDELEZWA

MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaanza kuliendeleza bonde la kilombero ili liweze kutunza maji na kuwasaidia wakulima wa eneo hilo kufanya kilimo cha uhakika.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo Agost 5 wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali.
Mhe. Rais amesema kupitia bonde hilo litasaidia kukusanya maji ambayo kwa kipindi cha kiangazi yatawasaidia wakulima kufanya kilimo cha umwagiliaji hadi kufikia kulima kwa misimu miwli kwa mwaka, pia hatua hiyo itapunguza upotevu wa maji ambayo kutokana na uwingi wake yanasababisha uharibifu wa miundombinu katika mkoa huo.