NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANA HANDENI

 

NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANA HANDENI

NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANA HANDENI

Wakazi wa Vijiji vya Msomera na Mkababu Wilayani Handeni Mkoani Tanga, ni miongoni mwa wanufaika wa kampeni ya Mhe Rais Dkt Samia ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake hao wamepongeza juhudi za  Mhe.Rais Samia katika uzinduzi wa kampeni hiyo, wakisema licha ya kuwa ni mpya, tayari imeonesha mafanikio makubwa kutokana na mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.
Kwa mfano huu ni mwezi wa tatu tangu nianze kutumia gesi, nimejiuliza maswali mengi na kujilaumu kwanini nilichelewa kuanza kutumia gesi kupikia nyumbani. Kweli nimepata manufaa mengi,” amesema Teresia Simon, mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Msomera, mtu wa jamii ya Kimasai.
Bi Mariam Khatib kutoka Kata ya Chang’ombe anasema kuwa kinyume na matarajio yake nishati hiyo ya gesi imempa nafuu ya maisha kwani kwa sasa anaweza kupika chakula chake haraka hasa wakati wa kuandaa chakula kwa ajili ya watoto wake kwenda shule.
“Sina tatizo tena la kuendelea kuhangaika na kuni wakati natakiwa kuwaandalia watoto wangu chakula na kwenda shule. Aina ya nishati imenipa ahueni nyingi. Pia nimehakikisha inapoisha naijaza mara moja kwa sababu nimegundua ni nishati inayookoa muda na mambo mengi ya nyumbani na kuniwezesha kufanya kazi nyingine,” amesema Mariam Khatib.
ZINGATIA:- Serikali inalenga ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watu wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.