HOSPITALI YA BUMBULI KUANZA KAZI MWEZI UJAO

 

HOSPITALI YA BUMBULI KUANZA KAZI MWEZI UJAO

HOSPITALI YA BUMBULI KUANZA KAZI MWEZI UJAO

TANGA
Hospitali mpya ya Halmashauri ya Bumbuli iliyojengwa wilayani Lushoto mkoani Tanga, inatarajia kuanza kazi Septemba 1 mwaka huu, huku shilingi bilioni 1.5 zikitumika kukamilisha ujenzi huo.
Uwepo wa hospitali hiyo ni faraja kwa wananchi wa Bumbuli kwani hapo awali, wakazi wengi walilazimika kusafiri hadi Lushoto au Korogwe kwa ajili ya huduma za rufaa, au kutegemea hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ya Bumbuli.
Pia hospitali hiyo mpya itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ambayo kwa sasa inahudumia majimbo ya Lushoto na Mlalo.