DKT SAMIA AHIMIZA UKUZAJI WA VIPAJI
ZANZIBAR
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendeleza vijana wenye vipaji ili kuvikuza na kuleta tija kwa Taifa.
Mhe Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akiweka Jiwe la Msingi Suluhu Sports Academy Mkunguni- Kizimkazi Zanzibar Agosti 22, 2024
Dkt Samia amesema “ Tanzania tuna vipaji tofauti tofauti ambavyo tukiviendeleza tutazalisha wanamichezo wazuri sana”
Pia Mhe Rais Dkt Samia ametoa agizo kwa Tff na Zff kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa viwanja Arusha na Dodoma pia uwanja wa Suluhu sports Academy, Zanzibar ili kuendana na muda uliobaki kuelekea mashindano ya Afcon.
“Tff na Zff muwe hapa kila mara,muangalie mambo yanavyokwenda, muangalie tunawezaje kukiingiza kiwanja hiki”amesisistiza Dkt Samia.