DKT SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO WA 44 WA SADC
DAR ES SALAAM
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Agosti 15 anatarajia kusafiri kuelekea Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 44 wa wakuu wa Nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 17 Agosti 2024.
Aidha katika mkutano huo Rais Samia atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya siasa,ulinzi na usalama ya SADC ambapo atapokea nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema anaemaliza muda wake.