DKT SAMIA AONGEZA UZALISHAJI WA TUMBAKU

 

DKT SAMIA AONGEZA UZALISHAJI WA TUMBAKU

DKT SAMIA AONGEZA UZALISHAJI WA TUMBAKU

TANZANIA
Wakati Mhe Rais Dkt Samia anachukua madaraka ya u-Rais Machi 2021 Tanzania ilikuwa inazalisha tani 65,000 za tumbaku na sasa (2024)  nchi inazalisha tani 122,000 na kuiwezesha kushika namba mbili Afrika kwa uzalishaji  wa tumbaku (nyuma ya Zimbabwe).
Aidha Dkt Samia akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kiwanda Cha Sigara Cha Serengeti, kilichopo mkoani Morogoro mapema mwezi Agosti amesema tumbaku yote itakayozalishwa na wakulima mashambani itanunuliwa.
“Sasa wakulima wataondokana na ‘grade’ ya uuzaji wa tumbaku kiwandani, maana nchi yetu sasa haitabakiza tumbaku majumbani kama zamani na kukuza uchumi wa wakulima na nchi yetu,” amesema Dkt Samia.
Hatua hiz zimepigwa kutokana na  uamuzi wa Mhe. Rais  Samia kusafiri nje ya nchi kwa lengo la kushawishi wawekezaji.
Aidha nchi sasa inavuna zaidi ya shilingi trilioni 1 kutokana na usafirishaji wa tumbaku duniani.