FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BRT INAYOENDELEA

 

FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BRT INAYOENDELEA

FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BRT INAYOENDELEA

DAR ES SALAAM
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka  (Mwendokasi/BRT) awamu ya Pili Jijini Dar es Salaam unaohusisha Lot ya kwanza ,ya pili na ya tatu.
Lot ya kwanza inahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3 kutoka Mbagala hadi Mzunguko wa Bandari uliopo eneo la Bendera Tatu,  Bendera Tatu hadi Kariakoo, Sokoine hadi Zanaki, barabara ya Kawawa hadi Magomeni na barabara ya Chang’ombe hadi Barabara ya Kilwa.
Lot ya pili inayohusisha ujenzi wa majengo ikiwemo vituo viwili, yadi moja na vituo mlisho(feeder stations) vinne umekamilika.
Vilevile, Awamu ya Tatu ya ujenzi wa barabara inayoishia Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.3 unatekelezwa na utakapokamilika  utapunguza msongamano na hatimaye kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Dar es salaam.