VIVUKO VITANO KUKAMILIKA SEPTEMBA 2024
MWANZA
Ujenzi wa vivuko vipya vitano vinavyoendelea kujengwa na Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mkoani Mwanza unatarajiwa kuanza kukamilika ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.
Vivuko hivyo ni Buyagu –Mbalika (75%) , Nyakarilo Kome (75%) wakati vivuko vya Ijinga Kahangala, Kisorya Rugezi na Bwiro Bukondo vimefikia 85% ya ujenzi wake.
Vivuko hivyo vipya vitakapokamilika vitakwenda kutoa huduma kati ya maeneo ya Ijinga na Kahangala Wilayani Magu, Bwiro na Bukondo Wilayani Ukerewe, Nyakaliro na Kome Wilayani Sengerema, Buyagu na Mbalika Wilayani Sengerema pamoja na Kisorya Wilayani Bunda Mkoani Mara na Rugezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.
