SERIKALI KUJENGA KIVUKO MAYENZI NA KANYINYA

 

SERIKALI KUJENGA KIVUKO MAYENZI NA KANYINYA

SERIKALI KUJENGA KIVUKO MAYENZI NA KANYINYA

KAGERA
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inatarajiwa kuanzisha huduma ya kivuko kwa wakazi wanaoishi eneo la Mayenzi kata ya Kibimba Tarafa ya Nyamiyaga na Kanyinya kata ya Mbuba Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara Mkoani Kagera.
Serikali imeamua kupeleka kivuko katika eneo hilo ili kiweze kutumika kuvusha wananchi wa Tarafa ya Rulenge na Tarafa ya Nyamiyaga na kusema ambapo kivuko hicho kitawasaidia wananchi kutoka upande wa kijiji cha Kanyinya kufika kwa urahisi eneo la Ngara mjini kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kijamii tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kuzunguka umbali mrefu kufuata huduma hizo.