DKT SAMIA APOKEA TAARIFA YA KITUO CHA KUPOZEA UMEME INYONGA
KATAVI
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Julai 13 ametembelea kituo cha cha kupokea na kupoza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme ya msongo wa kilovoti 132 wenye urefu wa Km 383 huku ukigharimu fedha Bilioni 116 na Bilioni 46.9 kwa ajili ya vituo vya kupozea umeme Inyonga na Mpanda huku wananchi wakilipwa fidia fedha Bilioni 5.378 kupisha mradi huo kwenye maeneo yao.
#TUPOKATAVI