TSH BIL 410.81 KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI KATAVI
KATAVI
Mkoa wa katavi unatekeleza miradi 8 ya kimkakati na ya kitaifa yenye thamani shilingi bilioni 410.81.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mpanda-Tabora (km 337.429), sehemu ya pili ni Komanga-Kasinde ( Km 108), pamoja na barabara ya Kasinde-Mpanda (Km 105.389) ambayo imeshakamilika.
Miradi mingine ya kimkakati na ya kitaifa inayoendelea kutekelezwa mkoani Katavi ni pamoja na barabara ya Mpanda-Uvinza-Kanyani (km 250.44), Kibaoni- Sitalike, sehemu ya Kibaoni-makutano ya Mlele (km50), barabara ya Kagwira-Karema (km 110.29), ujenzi wa kitanda cha Daraja la Kavuu (urefu wa mita 87.5)
#TukutaneKatavi