NCHI INA VIWANDA VITATU VYA KUSINDIKA NGOZI
TANZANIA
Hadi kufikia Aprili, 2024 Tanzania imeripoti kuwa na viwanda vitatu (3) vinavyofanya kazi ya kusindika ngozi ambavyo ni Himo Tanners and Planters (Kilimanjaro), ACE Leather (T) Ltd. (Morogoro) na Phiss Tanners (Pwani).
Viwanda hivyo vinasindika jumla ya vipande 198,100 vya ngozi ya ng’ombe na 717,000 vya ngozi ya mbuzi na kondoo vyenye thamani ya Shilingi bilioni 21.5.
Aidha, serikali imefanikiwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa malighafi bora kwa kuwaunganisha wamiliki wa viwanda vya kusindika ngozi na wazalishaji wa ngozi.
Pia jumla vya vipande 10,550 vya ngozi ya ng’ombe na 409,229 vya kondoo na mbuzi vilivyosindikwa hadi hatua ya kati (wet blue) vimeuzwa katika nchi za Pakistan na Ethiopia kwa thamani ya Shilingi 860,315,600.