“NUNUENI MAHINDI TSH 700 KWA KILO” DKT SAMIA
RUKWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya kilimo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuongeza bei ya kununua mahindi iwe shilingi mia saba kwa kilo kutoka bei ya awali ya shilingi mia sita kama alivyoagiza akiwa Mkoani Katavi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa Dkt Samia amesema “Pamoja na kupandisha bei nikiwa Katavi kuwa mia sita , nimekuja Rukwa bado malalamiko ni bei, nakuagiza waziri nendeni na bei ya mia saba kama wakulima walivyoomba”
Aidha Mhe Rais Dkt Samia amesema kutokana na wakulima kulalamikia bei ya mbegu za mahindi msimu ujao wa kilimo serikali itoe mbegu hizo kwa ruzuku “ Katika kituo kimoja wakulima walilalamikia bei ya mbegu za mahindi, sasa hebu tufanye kwa majaribio msimu ujao wa kilimo tutoe mbegu za mahindi na mbolea zote zije kwa ruzuku”Amesema Dkt Samia.