TSH BIL 2.9 KUJENGA CHUO CHA AFYA VWAWA
SONGWE
Ujenzi wa chuo cha Afya Vwawa Mkoani Songwe utaanza Oktoba, 2024 ambapo kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga jumla ya Tsh: Bilioni 2.9 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kupitia fedha za mradi wa Mama na mtoto kwa ajili ya kujenga jengo mseto (Academic complex).
Hadi sasa tayari utaratibu wa kupata eneo umefanyika ambapo kiasi cha shilingi Milioni 151 kimetumika kwa ajili ya kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliopisha eneo hilo.
Aidha chuo hicho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stahashada (Diploma) kwa kozi za uuguzi pamoja na kozi nyingine ambazo ni muhimu katika utoaji wa huduma za Afya ikiwemo wataalam wa maabara.