TSH MIL 89+ ZAWAPA KICHEKO WANA-KOROGWE
TANGA
Kiasi cha Shilingi Milioni Themanini na Tisa na Laki Nne zimewapa kicheko wazazi, walezi na wanafunzi wa kata ya Mtonga kwa kujengewa Vyumba vitatu vya Madarasa na Matundu nane ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Semkiwa iliyopo kata ya Mtonga Mjini Korogwe Mkoani Tanga.
Fedha zote za utekelezaji wa Mradi huo zimetolewa na Serikali kwa lengo la Uboreshaji wa Sekta ya Elimu hapa nchini.