SHULE 100 ZA ELIMU YA UFUNDI KUJENGWA NCHINI
DAR ES SALAAM
Tanzania inaanza mpango wa mageuzi wa kujenga shule 100 za sekondari za elimu ya ufundi maalumu nchi nzima, kwa lengo la kukuza ujuzi na ukuaji wa uchumi.
Hatua hii, ni sehemu ya dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya mfumo wa elimu unaozingatia ujuzi, inayolenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa vitendo pamoja na maarifa ya kitaaluma.
