SEKTA YA VIWANDA KINARA USAJILI WA MIRADI
DAR ES SALAAM
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema katika mwaka wa fedha uliopita sekta ya viwanda iliongoza katika sekta nyingine za kiuchumi kwa kuvutia wawekezaji zaidi kwa kusajili miradi 313 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.5 (kama trilioni 6.6/-), ikifuatiwa na uchukuzi iliyorekodi 128 miradi yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1 (karibia sh.tril 2.7).
Sekta nyingine katika orodha hiyo, kwa mujibu TIC ni mali isiyohamishika ya kibiashara ambayo ilivutia miradi 76 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 (karibia trilioni 2.7/-), sekta ya utalii yenye miradi 75 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 349 (zaidi ya bilioni 900/-) na kilimo ambacho kilirekodi miradi 56 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 710 (kama trilioni 1.9/-).
Sekta ya utalii iliipita sekta ya kilimo kwa kusajili miradi mingi zaidi huku filamu iliyorekodiwa na Mhe Rais Dkt Samia (Royal Tour) ikiwa sababu kuu iliyochangia sekta ya utalii kuvutia wawekezaji wengi.
