MIRADI 707 YA TSH TRIL 19 ILISAJILIWA 2023/24
DAR ES SALAAM
Taarifa kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) inasema idadi ya miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa katika mwaka wa kifedha uliomalizika wa 2023/2024 ilifikia 707 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 7 (kama trilioni 19/-) ikilinganishwa na miradi 369 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.4 (tri/-) iliyorekodiwa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambayo ni sawa na 91% ya ongezeko la uwekezaji.
Asilimia 38 ya miradi yote iliyosajiliwa inamilikiwa na wawekezaji wa ndani, 43% ni Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDI) wakati 19% ni ya ubia
Usajili huo mkubwa wa miradi unatokana na mageuzi ya kimuundo na kisheria yanayosimamiwa na serikali ya awamu ya sita, hasa kupitishwa kwa Sheria Mpya ya Uwekezaji ya 2022,"
FAHAMU:- Sheria mpya ya Uwekezaji imekuwa ikichukuwa jukumu muhimu katika kuinua uwekezaji wa ndani kwa kupunguza kiwango cha chini cha mtaji wa uwekezaji hadi dola za Kimarekani 50,000 (milioni 133) kutoka dola 100,000 za Kimarekani ( milioni 267).
