SERIKALI KUONGEZA KASI NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 

SERIKALI KUONGEZA KASI  NISHATI SAFI YA KUPIKIA

SERIKALI KUONGEZA KASI  NISHATI SAFI YA KUPIKIA

TANZANIA
Katika mwaka 2024/25 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 – 2034 kwa kupatia ufumbuzi vikwazo vya matumizi ya nishati hiyo, ikiwemo gharama kubwa, upatikanaji hafifu na uhaba wa miundombinu yake na kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya nishati zisizo safi na salama za kupikia.
 Aidha Serikali kupitia Wizara ya nishati itaendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia inayolenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP)
Vilevile itaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko banifu kwenye Kaya zilizopo katika maeneo ya Vijijini, na Mijini, kutoa ruzuku kwa wazalishaji wa mkaa mbadala kwa ajili ya ununuzi wa mashine zitakazotumika katika uzalishaji wa mkaa huo, kuendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza katika ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupkia katika maeneo 211 pamoja na kuendelea na usambazaji wa gesi asilia majumbani, hususan katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani.