MIL 900 KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA, MLOWO
SONGWE
Serikali itapeleka shilingi Mil 900 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe kwa ajili ujenzi wa Kituo cha Afya Mlowo kitakachotoa huduma kama Hospitali ya Wilaya.
Ujenzi wa Kituo hiki utafanya Idadi ya Vituo vya Afya katika Wilaya ya Mbozi kufikia 6 na Kituo hicho kitawekewa vifaa tiba vyote muhimu ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora za Afya.
