MHE. RAIS SAMIA AMPONGEZA RAIS KAGAME

 

MHE. RAIS SAMIA AMPONGEZA RAIS KAGAME

MHE. RAIS SAMIA AMPONGEZA RAIS KAGAME

RUKWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais Mteule wa Rwanda Paul Kagame   Kufuatia  kutangazwa kuwa mshindi na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi  Rwanda Bi Oda Gasinzigwa baada ya uchaguzi uliofanyika Julai 15 mwaka huu nchini humo na kupata 99.15% ya kura zote zilizopigwa.
Kupitia ukurasa wa x na instagram Mhe Rais Samia ameandika
“On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency Paul Kagame, on being re-elected as the President of the Republic of Rwanda. I look forward to continue working with you in fostering the relations between our two countries and in the pursuit of East Africa’s unity and prosperity”
(Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Paul Kagame, kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Rwanda. Natarajia kuendelea kufanya kazi nanyi katika kukuza uhusiano kati ya nchi zetu mbili na katika kutafuta umoja na ustawi wa Afrika Mashariki).
Bimkubwa Tanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kumpongeza Rais mteule wa Rwanda Mhe Paul Kagame.