TAZAMA HAPA:https://www.youtube.com/watch?v=5WHB_Wqc2Fo
IJUE BANDARI YA KAREMA ILIYOPO MKOANI KATAVI AMBAYO IMEBORESHWA KWA KIASI CHA TSH BIL 47.97
Bandari hii ni miongoni mwa bandari 17 za Ziwa Tanganyika yenye ukubwa wa eneo la heka 66 kwa jumla ikiwa na miundombinu ya kisasa kulinganisha na bandari nyingine za ziwa Tanganyika na ndiyo bandari pekee iliyo jirani zaidi na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa umbali wa km 298 na bandari nyingine ni ya karemii ambayo iko umbali wa km 338 ambayo ni bandari maarufu ya nchi hiyo.
Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Karema ni Mpango wa Serikali kuimarisha miundombinu ya Bandari na kuboresha utoaji wa huduma kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji hapa nchini.