DKT SAMIA AFUNGUA JENGO LA KAMANDA WA POLISI
KATAVI
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Julai 14 amefungua jengo la kamanda wa polisi mkoani Katavi lenye thamani ya shilingi bilioni 1.4.
Jengo hilo lina jumla ya mita za mraba 1438 ambazo zimegawanyika katika sakafu nne zenye vyumba vya ofisi 33, vyumba viwili vya kuhifadhia silaha pamoja na kumbi 2 za mikutano pia jengo hilo limefungwa kamera 15 kwa ajili ya ulinzi na usalama.
#TupoKatavi