DKT SAMIA AONGEZA KIWANGO CHA ELIMU RUKWA
RUKWA
Jitihada zinazofanywa na Dkt Samia katika kuboresha sekta ya elimu nchini, zimezaa matunda kwa kuongeza Idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa katika ngazi mbalimbali za kujiunga na elimu katika mkoa wa Rukwa.
Katika kipindi cha uongoziwa Dkt samia na kufanya uwekezaji huo idadi ya wanafunzi walioandikishwa kujiunga na elimu ya msingi imeongezeka kutoka 46,526 kwa Mwaka 2021 hadi 63,666 kwa Mwaka 2024 sawa na ongezeko la 36% huku idadi ya wanafunzi waliojiunga na elimu ya Sekondari ikiongezeka kwa 9% kutoka wanafunzi 315,887 Mwaka 2021 hadi kufikia 346,787 kwa Mwaka 2024.
Kwa ujumla, Mkoa wa Rukwa umeshuhudia mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu katika kipindi cha Mwaka 2021 mpaka 2024. Mabadiliko hayo yanaithibitisha nia ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira bora ya kujifunza na kujifunzia ili kuinua kiwango cha elimu na ujuzi kwa wananchi.
#SisiTupoRukwa