TSH BIL 27.7 KWENYE MIRADI YA MAJI KATAVI
KATAVI
Kiasi cha Sh bilioni 27.7 kimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 40 ya maji mkoani Katavi katika kipindi cha 2021 hadi 2023 kwenye uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita , fedha iliyowezesha kununua pia mitambo ya kuchimba kisima hadi chenye urefu wa mita 400.
Lengo la kutolewa kwa kiasi hicho ni kufikisha 85% ya upatikanaji wa maji kabla ya kufika mwaka 2025.
#TukutaneKatavi