BIL. 83.1 ZATUMIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UENDELEVU (SRWSS)

 

BIL. 83.1 ZATUMIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UENDELEVU (SRWSS)

BIL. 83.1 ZATUMIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UENDELEVU (SRWSS) 

TANZANIA
Kiasi cha shilingi bilioni 83 kimetumika kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelevu wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS) huku sekta ya Afya ikitumia shilingi Bil. 54.39 na ujenzi wa miundombinu ya Elimu ikitumia shilingi Bil. 28.73.
Mradi  huo unatekelezwa katika mikoa yote  ya Tanzania bara na Halmashauri 137, huku Manispaa, miji na majiji ikiwa sio sehemu ya mradi huu.
Mpaka sasa mradi wa SRWSS umefikia vituo vya kutolea huduma za Afya 2,727 na shule za Msingi 1,842, kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 838 na shule 566 vimepokea fedha za utekelezaji.