KIWANJA CHA NDEGE MSALATO SASA NI 67.6%

 

KIWANJA CHA NDEGE MSALATO SASA NI 67.6%

KIWANJA CHA NDEGE MSALATO SASA NI 67.6%

DODOMA
Ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato mkoani Dodoma umefikia 67.6% kwa upande wa miundombinu ya njia ya kuruka na kutua ndege huku ujenzi wa jengo la abiria ukifika 32.21%.
Utekelezaji wa mradi huo unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa Kilometa 3 na mita 600 ambapo unagaharimu kiasi cha shilingi Bilioni 165.6 pamoja na ujenzi wa jengo la abiria  ambalo linagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 194.4.