“VYOMBO VYA HABARI VILIPWE KABLA YA DISEMBA 20” DKT SAMIA
DAR ES SALAAM
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara na taaasisi zote za umma zinazodaiwa na vyombo vya habari ndani ya serikali zihakiki madeni ya vyombo hivyo na kuhakikisha zinakubaliana namna ya utaratibu wa kulipana.
Dkt Samia ametoa agizo hilo leo Juni 18, 2024 akiwa kwenye kongamano la Maendeleo ya sekta ya habari lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam lililowakutanisha waandishi wa habari, wadau wa habari na maafisa habari wa serikali.
Amesema “wizara na taasisi za umma zinazodaiwa na vyombo vya habari ndani ya serikali zihakiki madeni hayo na zikubaliane namna ya kulipana , na jambo hili lifanyike si zaidi ya Disemba 20 mwaka 2024”
Aidha Dkt Samia ameongeza kwamba” tukivuka 2025 madeni mengi ya vyombo vya habari yanayolipika yawe yamelipwa,mimi nitasimamia ndani ya serikali yangu na hakikisheni nanyi madeni yenu yamekaa vizuri”.