“UHUSIANO KATI YA SERIKALI NA VYOMBO VYA HABARI UMEIMARIKA” DKT SAMIA
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uhusiano baina ya serikali na vyombo vya habari umeendelea kuimarika kutokana na uhuru wa vyombo vya habari uliopo kwa sasa nchini.
Mhe Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 18, 2024 wakati akizungumza kwenye kongamano la maendeleo ya sekta ya habari lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Dkt Samia amesema “ April 6 mwaka 2021 nilikutana na kubadlishana mawazo na wahariri wa vyombo vya habari ambapo niliwahakikishia kulinda uhuru wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla, leo hii najisikia fahari kwamba uhusiano baina ya serikali na vyombo vya habari unaendelea kuimarika” amesema Dkt Samia.
Aidha Dkt Samia amesema “Nimesoma taarifa ya taasisi ya vyombo vya habari kusini vya Afrika (MISA) ya mwaka 2023 kwenye taarifa iliyowasilishwa na Misa tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) kwamba uhuru wa vyombo vya habari nchini umeimarika sana katika kipindi hiki”.