VITUO VIPYA 311 (SARATANI) VYAANZISHWA

 

VITUO VIPYA 311  (SARATANI) VYAANZISHWA

VITUO VIPYA 311  (SARATANI) VYAANZISHWA

TANZANIA
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imefanikiwa kuanzisha vituo vipya 311 vya kutolea huduma za uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi na matiti hapa nchini na hivyo kufikia jumla ya vituo 1,308 ikilinganishwa na vituo 997 mwaka 2022/23. 
Aidha, katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 wanawake 2,827,088 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti ambapo 11,418 walionekana kuwa na viashiria vya saratani na kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 kati ya wanawake 2,459,498 waliofanyiwa uchunguzi 7,723 waligundulika kuwa na viashiria vya saratani.