WATOTO 9,456,436 WAPATIWA MATONE YA VITAMIN A

 

WATOTO 9,456,436  WAPATIWA MATONE YA VITAMIN A

WATOTO 9,456,436  WAPATIWA MATONE YA VITAMIN A

TANZANIA
Serikali kupitia wizara ya afya kwa mwaka wa fedha 2023/24 imewapatia Jumla ya watoto 9,456,436 matone ya vitamin A ambayo ni sawa na 99% ya lengo lililowekwa la kuwafikia watoto 9,460,369.
Kiwango cha utekelezaji kimeongezeka ikilinganishwa na watoto 9,052,340 waliofikiwa kipindi kama hicho mwaka 2022/23.
Huduma ya utoaji wa matone ya Vitamini A kwa watoto chini umri wa miaka 5 hufanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa utaratibu wa kawaida ambapo mtoto akitimiza umri wa miezi 6 hupewa matone ya vitamini A na huendelea kupatiwa matone hayo kila baada ya miezi 6 hadi atakapotimiza umri wa miaka 5.