MADARAJA 14 KUJENGWA
TANZANIA
Serikali imetafuta wakandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Madaraja sita (6) ya Mirumba (Katavi), Mpiji Chini (Dar es Salaam), Simiyu (Mwanza), Sukuma (Mwanza), Kibakwe (Dodoma), Kerema Maziwa (Dodoma).
Pia serikali inaratibu manunuzi ya wakandarasi wa ujenzi wa madaraja nane (8) ya Sanza (Singida), Mkenda na Mitomoni (Ruvuma), Godegode na Nzali (Dodoma), Doma, Chakwale na Nguyami (Morogoro) .
Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja ya Malagarasi Chini (Kigoma) na Munguli (Dodoma) unaendelea.