VIVUKO 19 VYABORESHWA

 

VIVUKO 19 VYABORESHWA

VIVUKO 19 VYABORESHWA

TANZANIA
Serikali kupitia wizara ya ujenzi inatekeleza miradi ya usimamizi wa mafuta na usimikaji wa mifumo ya kielektroniki katika vivuko 19 ambavyo ni Mv. Kazi, Mv. Kigamboni, Mv. Kilindoni, Mv. Misungwi, Mv. Sengerema, Mv. Mwanza, Mv. Sabasaba, Mv. Ilemela, Mv. Mara, Mv. Chato Ii, Mv. Tegemeo, Mv. Temesa, Mv. Kome Ii, Mv. Musoma, Mv. Ujenzi, Mv. Tanga, Mv. Pangani Ii, Mv. Kilambo Na Mv. Mafanikio.
Aidha ujenzi wa maegesho ya Mayenzi – Kanyinya (Ngara) umefikia 80%, Ijinga - Kahangala (Magu) umefikia 48%, Izumacheli (Chato – Nkome) umefikia 95%, Mlimba – Malinyi upande wa Mlimba umefikia 40% na upande wa Malinyi umefikia 85% pamoja na maegesho ya Bwiro – Bukondo (Ukerewe).
Aidha mikataba ya ujenzi wa maegesho ya Kisorya – Rugezi, Kahunda – Maisome na Ilunda - Luchelele imesainiwa na ipo katika hatua za awali za kuanza utekelezaji.